Habari hii nayo niliikuta katika jumba la Macha, na ikanivutia sana tu kwasababu inanigusa kwa kila hali. Ni kuhusiana na Uhuru wa Vyombo vya Habari. Kwa mujibu wa masimamo wa “ligi” ya Uhuru wa vyombo vya Habari, Duniani, uliotolewa na Shirika la Wana-Habari wasio na mipaka, Tanzania ni nchi ya 88, ikiwa imezidiwa hata na Liberia, ambayo ni ya 84 (Macha, naomba urekebishe kidogo hapo).
Nchi zilizoshika nafasi tatu za juu ni Finland, Iceland na Ireland, huku nchi za tatu kutoka chini zikiwa ni Korea Kaskazini, Turkmenistan na Eritrea. Maswali ambayo yalitumika katika kuandaa ripoti hiyo yalikuwa haya, na upangiliaji wa ripoti yenyewe baada ya kukusanywa kwa majibu ya maswali hayo ulikuwa huu hapa.
Lakini pengine sehemu ambayo sisi wanahabari wote kwa ujumla wetu, mahali na wakati wowote ule tunatakiwa kupawekea mtizamo wa kipekee, ni kwenye taarifa za yanayoendelea nchini Libya, ambako inadaiwa eti ni aheri kumpinga Mungu ukiwa mwanahabari huko, kuliko kumwandika vibaya rais wa nchi hiyo, yaani komredi Muammar Gaddafi
October 30, 2006 at 11:04 am
Msangi, sijakuelewa…… Gaddafi huyu huyu ambaye kwa sasa anaonekana kama kinara wa kuiunganisha Afrika? Habari hii imenisisimua sana kwakweli
November 28, 2009 at 3:36 pm
Swali la james ni langu pia! How blind are we au ni utaratibu wa viongozi wa afrika wa kuoneana aibu. kila siku wanazungumza kuhusu kuunda umoja na umoja uliotengana