Inawezekana kabisa hata Mwaipopo ambaye ni kwao hajawahi kufika, lakini mimi mgeni nimepatembelea. Namaanisha kwenye kivutio kimoja wapo cha utalii kati ya vingi ambavyto viko Mbeya. Hicho ni Kimondo ambacho kinapatikana wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya, ambacho naamini wenhi wetu tulijifunza wakati tuko mashuleni.