najua mmenikosa sana ndugu zangu, kama ambavyo nami nimewakosa sana, lakini naomba niwahakikishie kuwa muda si mrefu tutakuwa wote tena kwa ukaribu sana. Wajua hii Tanzania yetu, kuna baadhi ya maeneo ambako bado ni Tanganyika, na hasa kwa upande huu wa hii teknolojia ya mawasiliano ya mtandaoni. Nimekumbwa na hitilafu kidogo katika njia ya kunifikishia mawasiliano ya mtandao mahali nilopo hali ambayo inanikosesha wakati wa kutosha kuendeleza hili gurudumu la ku-blogi.
Nawashukuru sana nyote mnaonikumbuka na ninawaahidi kuwa tuko pamoja daima, kwa kasi ile ile, ari ile ile na nguvu zile zile
February 22, 2006 at 10:20 am
Hongera
kwangu tu ni kuweza kuwapongeza kwa kuweza kulidumisha na kuliendesha lugha yetu ya Kiafrika hasa katika mtandao. Tuendelee vivyo hivyo hili lugha yetu ya Kiafrika isibaki nyuma. Hii ndiyo lugha inayotuunganisha tukiwa Wafrika hasa katika Afrika Mashariki.
February 23, 2006 at 8:45 pm
tumekusamehe
February 28, 2006 at 2:02 am
Pole kwa kutindikiwa na huduma ya Internet. Vipi kwa Desai karibu na NMB, au Mnasi communications, au Mafiati kwa Pangamawe, au Posta wameacha kutoa huduma hii?
March 4, 2006 at 12:42 am
Mwaipopo naona homa ya nyumbani imeanza kukupata.
March 5, 2006 at 12:56 pm
Msangi, tunazikosa tafakuri zako! mungu atusaidie mambo yarudi mahala pake!
March 8, 2006 at 10:20 am
Msangi, kichwa chako cha habari kinanifikirisha. Fafanua kidogo.
March 17, 2006 at 2:12 pm
Msangi, heding inahitaji waraka kamili. Nadhani kuna falsafa kubwa mumo.–>