vidume

Ukweli ni kuwa hawawezi kuwa sawa na wale wa kwetu wa kule TMK, lakini hakika Liverpool ni vidume vya shoka. Kutoka nyuma ya goli tatu hadi kushinda kombe la UEFA, katika fainali ya aina yake iliyokuwa imejaa ufundi wa hali ya juu namna ile, halikuwa jambo la kawaida. Lakini wakati tukiwapongeza kwa ushindi huo, sisi Watanzania, na hasa viongozi wetu wa vilabu na vyama mbalimbali vya soka nchini TUMEJIFUNZA NINI?