Napenda kwanza nikiri kuwa nimeandika kazi hii kutokana na kazi ya Bw. Ezuckerman, ambayo aliiandika katika Global Voices. Unaweza kuusoma waraka wake huo kwa kubonyeza hapa. Kuna mambo mengi sana ambayo aliyazungumzia katika waraka wake, lakini kuna baadhi ambayo yalinivutia sana. Licha ya kuonyesha kukubali kwake jitihada za watanzania katika kublogu kwa kutumia lugha ya Kiswahili, alikuwa na mambo kadhaa ambayo mbali ya sisi kuweza kumjibu, bilashaka yanatakiwa kuwa changamoto mpya kwetu sisi.

Kwanza alibaini kuwa sehemu kubwa ya Wanablogu wa Kitanzania ni waandishi wa habari, akajiuliza je hilo linamaanisha nini?, Pili alibaini kuwa karibu wote wamekuwa wakijadili zaidi masuala ya Kisiasa, je hakuna mambo mengine ambayo wanaweza kujadili zaidi ya hayo?

Kwa kuanzia, labda nadhani nianze kuwauliza wanablogu wenzangu wa Kitanzania swali hili, Je, Hayo mawazo ya Bw. Ezuckerman, yanamaanisha nini kwetu sisi? Kisha tutaendelea zaidi kwa kuanzia hapo.