Ninachomaanisha hapa ni Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, ndugu zangu. hakika ni juhudu kubwa sana ambazo zimekuwa zikifanywa na Watanzania katika kuhakikisha kuwa walau tunaongeza kasi ya kuwafukuzia wenzetu ambao tayari walishatutangulia maili kadhaa siku zilizopita. Baada ya kuwepo kwa Watanzania kadhaa ambao wamekuwa wakiblogu katika lugha ya Kiswahili, hivi sasa wameamua kuanza kubobea zaidi kwa kutumia lugha za makabila ya Kitanzania. Kwa kuanzia, yupo binti aliyeko Marekani, ambaye ameamua kublogu klwa kutumia lugha ya Kichaga. Huyu ni ANNETH ASSENGA. Hebu msome hapa

.