Kuna mmoja kati ya wasomaji wangu aliye Canada ambaye aliniuliza kuwa ni namna gani anaweza kunipata pamoja na kuhitaji pia kutambua vizuri Tanzania iki namna gani. Kwa manufaa yake yeye binafsi pamoja na wengine wote ambao bado walikuwa hawaijui vyema Tanzania, nimeanzisha kolamu maalum kwa ajili ya kuwawezesha wasomaji wangu kutambua baadhi ya mambo ya msingi kuhusiana na nchi yangu. naamini kuwa wakishamaliza kusoma hapo watakuwa katika nafasi nzuri ya kuweza kuja nitembelea au hata kutalii Tanzania. Karibuni Tanzania