Kutokujadiliwa kwa rufaa ya Mzee wa ushindi, kutupiwa virago kwa baadhi ya wachukua fomu na kisha wakakaa kimya kinyume na wengi tulivyokuwa tukidhania huku pia wengine wakijitoa, ni baadhi tu ya vijambo (sio mbwembwe), vilivyojiri mjini Dodoma wakati wa vikao vya ‘Baraza la Makadinali wa CCM’, vya kuelekea kumsaka ‘Mtakavitu Papa Wao’ (wangapi sijui). Katika siku za karibuni, nitawaletea mlolongo mzima wa matukio yaliyojiri mjini hapa, kuanzia siku ya kwanza hadi siku ambayo hatimaye, kutoka katika Sestine yao (Chimwaga), tuliweza kusikia Habemus Candidati