Dalili za moshi wenye rangi mchanganyiko (Kijani na Njano), kufuka zinazidi kukaribia sasa, lakini kama nilivyowahi kutanabaisha awali, ni baada ya kutanguliwa na “mmwagiko wa damu”. Hii ni baada ya vikao vya siku mbili vya kamati kuu na halmashauri kuu ya ‘Baraza la Makadinali’ wa CCM, ambavyo sasa vinaelekea kutupatia jina la mtu ambaye watamtawaza kama ‘Papa’ wao.

Baada ya vikao vya kamati kuu na hatimaye halmashauri kuu ya CCM, kukutana jana na juzi mjini Dodoma, hatimaye wagombea watatu ambao watachujwa leo hii na hatimaye mmoja wapo kutajwa kama mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya chama hicho, wamepatikana na leo hii, wawili kati yao wanatarajiwa kuchujwa zaidi ili kumpata mmoja ambaye atatawazwa kuwa ndiye mgombea, na bilashaka atakayekuja kuwa mwenyekiti wa chama hicho katika siku za karibuni. Unajua ilikuwaje? Soma hapa