Poleni sana ndugu zangu ambao mmekuwa mkiusubiri kwa hamu sana Moshi utakaoufuka kutoka katika Sestine ya wana-CCM (Chimwaga), kujua kuwa utakuwa wa namna gani. Najua ni kwa kiasi gani mmekuwa na hamu sana ya kujua moshi huo utakuwa wa aina gani, mwekundu, mweusi, kijani, njano au cheche kama ninavyoamini mimi; lakini jambo moja ninalowaombeni mtambue ni kwamba, moshi huu mnaousubiri bwana sio sawa na ule wa Vatican.

Huu ni moshi ambao ili uweze kutoka ni lazima kwanza “damu imwagike”. Unashangaa!. Waliokuwa wamenunua (Kuchukua??), fomu ni watu 11, kati ya hao ni mmoja tu ambaye anatakiwa, unadhani hawa wengine watafanywa nini?. Kuchinjiwa baharini, kama wenyewe wanavyoita zoezi hilo la mchujo, ndio maana nawaambia kuwa subira yenu ni muhimu sana kwasababu ni lazima ‘damu’ za watu 11, zimwagwe baharini kwanza ndio moshi uweze kutoka.

Kwamba moshi utakuwa wa aina gani, hilo ni swali jingine kabisa lakini ni lazima utoke na ni lazima kwanza utanguliwe na kumwagika kwa damu za watu watakaochinjiwa baharini. Wakati naandika kaujumbe haka, tayari sita wameshachinjiwa baharini zamaaaaani sana, na tunasubiri wengine wawili kisha wawili tena ili tumpate mmoja na mgombea mwenzake.

Kigumu Chama cha Mapinduzi