Unaweza kuiita vyovyote uwezavyo. Ni kashfa ya kwanza na ya aina yake kuwahi kuwakumba wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wale ambao ndio wamekuwa siku zote wakishiriki katika kujadili sheria mbalimbali za kuwabana ‘Wadanganyika’ ambao watabainika kuwa wametenda makosa mbalimbali kisheria. wale ambao tuliwapa dhamana na imani zetu zoooote wakatuwakilishe katika chombo hicho kikubwa cha kuunda sheria katika nchi yetu. Wale wale ambao, ilifikia wakati wakaamua kwa dhati kabisa kuhalalisha kuwa wao waitwe waheshimiwa.
Nawazungumzia wabunge watatu kutoka chama cha upinzani cha CUF, ambao waliamua kutumia madaraka yao kuudhalilisha umma wa ‘Wadanganyika’, kulidhalilisha Bunge letu tukufu na kuharibu kabisa imani na uaminifu waliojijengea Wadanganyika kwa zaidi ya miaka 40 iliyopita, katika jumuiya za kimataifa.Mmoja kati ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano ulioanika hadharani maovu yao aliandika hivi: Bonyeza hapa usome na utoe maoni yako kuhusu waheshimiwa hawa.