Katika kipindi hiki ambapo tunauelekea uchaguzi mkuu, pilika pilika kibao zenye lengo la kuchafuliana majina hasa kwa wawania nafasi ya kuwa wagombea ‘Urahisi’ kwa tiketi ya CCM, zimekuwa zikipamba moto kila kukicha.

Inavyoelekea ni kuwa wamesahau kabisa wajibu wao kuwa ni kutushawishi sisi kuwa wamefanya mambo gani kwa ajili ya kustahili kuwa mashujaa wa taifa hili na badala yake wameelekeza juhudi zao katika kuchafuliana majina. Watanzania kadhaa wamekuwa wakijiuliza kuwa mwisho wa hali hii ni nini hasa kama sio kulipeleka taifa sehemu mbaya?

Mmoja kati ya waandishi waandamizi wa gazeti moja la kila wiki ambaye sipendi nimtaje kwakuwa sijaomba ridhaa yake amesema haya, kuhusiana na hali hii “Silaha ya kupandikiza ubaguzi na chuki katika jamii ni silaha mbaya na ya maangamizi kwa jamii, tunayo mifano hai juu ya hilo”
Hakika maneno haya yanatakiwa kufanyiwa kazi kimamilifu